Loading...

"MAFANIKIO HAYAPATIKANI KWA USINGIZI MMOJA" - Na Siri ya Utajiri

Loading...
Vince Lombardi  anayeaminika kama kocha bora katika historia ya mpira wa miguu huko marekani  aliwahi kusema "Ukimuona mtu juu ya kilele cha mlima usifikiri kwamba mtu huyo kajikuta tu katika kilele hicho. 

Vince Lombardi kama kocha mkuu katika timu ya Green Bay Packers aliiongoza timu yake katika ushindi kwa miaka saba na kubaki kama kocha na kiongozi wa mfano katika ligi ya marekani. 

Alikusudia kusema nini?  Mafanikio yake hakuamka asubuhi akakuta ameyapata, alifanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa. Alikutana na changamoto mbalimbali lakini alisimama na kushikilia dhamira yake ya kufanikiwa. Alikuwa tayari kutumia uwezo wake wote na mbinu zote ili kufanikisha ushindi wa timu yake.

Nawe ili uweze kufika katika kilele cha mafanikio yako katika jambo lolote lazima uwe tayari kujitoa na kuvumilia kupanda mlima. Katika safari ya kupanda utakutana na mawe, miba, uchovu na kila aina ya changamoto. Hakuna namna lazima uendelee kusonga mbele bila kukata tamaa.

You Deserve The Best!
Vicent Stephen
"MAFANIKIO HAYAPATIKANI KWA USINGIZI MMOJA" - Na Siri ya Utajiri "MAFANIKIO HAYAPATIKANI KWA USINGIZI MMOJA" - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 2/08/2018 10:13:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.