Loading...
Tunapoianza wiki nyingine mpya usisahau kuainisha malengo yako ya wiki nzima. Kama hujatengeneza hujachelewa sana, hakikisha kabla siku ya leo haijaisha uwe tayari umeshaanda mpango wako wa wiki nzima.
Kumbuka pia kuwa na malengo haya pekee haitoshi kukusaidia. Jambo la msingi ambalo ni muhimu sana katika yote ni NIDHAMU ya malengo na mpango uliojiwekea.
Bila NIDHAMU ya kutii malengo yako ni rahisi sana kusahau ulichokipanga na kujikuta umeangukia katika mambo ambayo sio sehemu ya malengo yako.
Dunia imejaa kila namna ya ushawishi ambao ni rahisi sana kukuondoa katika mpango wako. Pamoja na vishawishi hivi lakini bado una uwezo wa kusema HAPANA.
NIDHAMU ya kutii malengo yako ndio silaha pekee ambayo itakuhakikishia kufanya kile ulichokusudia. Wiki hii jitahidi kusimama na malengo yako. Usiruhusu kusaliti malengo uliyojiwekea.
You Deserve The Best!
Vicent Stephen
KUWA NA MALENGO PEKEE HAITOSHI, UNAHITAJI PIA NIDHAMU YA KUTII MALENGO HAYO - Na Siri ya Utajiri
Reviewed by By News Reporter
on
2/05/2018 02:11:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: