Loading...
Mwimbaji wa miondoko ya pop Madonna amemuita mwanae, David Banda, "Rais wa baadae wa nchi ya Malawi" kupitia mtandao wa twitter alimnadi mtoto huyo wa miaka 12.
Mwimbaji huyo Mmarekani ana watoto sita, wanne kati yao aliwaasili kutoka nchi ya Malawi.
Kupitia mtandao wa twitter alisema: "Siku ya Rais, Ninasherehekea Rais wa baadaye wa Malawi?? Kipenzi cha Waafrika. ?"
Ingawa Madonna aliripoti ana mahusiano mazuri na uongozi wa nchi ya Malawi hapo nyuma. Mwaka 2013, Malawi ilimtuhumu Madonna kwa "Kuwadhulumu viongozi wa kiserikali" kwa kigezo cha kuonyesha mchango mkubwa katika nchi hiyo, hivyo anapaswa kugewa huduma kama mheshimiwa wa ngazi ya juu.
Maneja wa mwimbaji Madona pia aliituhumu nchi ya Malawi kwa kuwa na kinyongo na hisani aliyotoa mwimbaji huyo.
Ila mwaka jana, Malawi ilimpa ruhusa Madonna kuwaasili watoto wawili na akawa mama wa watoto mapacha ambao ni Esther na Stella Mwale.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MADONNA AMTABIRIA MWANAE URAIS WA NCHI YA MALAWI
Reviewed by By News Reporter
on
2/21/2018 10:53:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: