Loading...
Maafisa wa forodha nchini Kenya wamemkamata mwanamume anayedaiwa kuwa raia wa Tanzania katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi akisafirisha dhahabu ya thamani ya dola milioni moja, taarifa zinasema.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 46 anadaiwa kuwasili kutoka Mwanza, Tanzania kupitia uwanja wa Kilimanjaro na alikuwa safarini kuelekea Dubai.
Gazeti la kibinafsi ya Nation linasema mwanamume huyo, ambaye jina lake halijafichuliwa kufikia sasa, aliwasili uwanja wa JKIA Ijumaa 16 Februari alishuka na ndege ya Precisious Airlines akitokea Tanzania na alitaka kupanda ndege ya Kenya Airways kuelekea Dubai.
Maafisa wa Idara ya Uchunguzi wa makosa ya Jinai wakiandamana na maafisa wa uchunguzi kutoka Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) walimhoji na akaandikisha taarifa.
Kwa nini akakamatwa?
Sheria za Usimamizi wa Forodha za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za mwaka 2004, Kifungu 85(3) na Kiambatisho cha Pili Sehemu B (4) huharamisha usafirishaji wa madini ambayo hayajapitia viwandani katika kanda ya Afrika Mashariki.
Vipande hivyo vya dhahabu vya uzani wa kilo 32.3 vinashikiliwa na maafisa wa idara ya forodha wa KRA huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
MTANZANIA AKAMATWA NA DHAHABU YENYE THAMANI YA DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 1
Reviewed by By News Reporter
on
2/21/2018 12:00:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: