Loading...
Mzaliwa wa Uganda na muigizaji wa Kiingereza Daniel Kaluuya ameshinda tuzo ya BAFTA kama msanii chipukizi baada ya kuonekana kuigiza kwa umahiri kupitia filamu ya 'Get Out'.
Muigizaji huyo wa miaka 28 aliwashinda waigizaji kama Florence Pugh, Josh O'Connor, Timothee Chalamet na Tessa Thompson kwa idadi ya kura zilizopigwa na washiriki.
Akishukuru wakati akipokea tuzo aliwapongeza washariki wenzake ikiwa pamoja na kumshukuru mwalimu wake wa uigizaji na familia yake kumpa ruhusa ya kufikiria tofauti.
Tukio linazidi kuwapa hamasa waigizaji wa Uganda na Afrika Mashariki kiujumla kwamba wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwani hakuna kinachoshindikana, na 'kufikiria tofauti' kutakupandisha kilele cha mafanikio yako.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MGANDA ALIYESHINDA TUZO ZA BAFTA
Reviewed by By News Reporter
on
2/21/2018 12:29:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: