Loading...

MLA NYAMA ZA WATU AKAMATWA NA POLISI

Loading...
dundiika news blog
Polisi nchini Msumbiji katika kijiji kimoja huko Magharibi ya jiji la Tete wamemkamata mtu aliyetuhumiwa kwa kula nyama za watu, baada ya wakazi wa eneo hilo kumkuta na nyama ya mtu iliyotambulika ni ya mtoto mdogo, mwili wa mtoto huyo uliotambulika inasemekana aliufukua katika makaburi ya Chimadzi, Tete.

Unyama huo uliogundulika uliwakasirisha wananchi ambao walitaka kumuua mla nyama za watu na hatimaye kuokolewa na polisi.

Msemaji Mkuu wa polisi Jiji la Tete, Lurdes Ferreira, amemtaja mtu huyo kama Rui Foia, na amethibitisha kuwa yeye na aliyehusika na ufukuaji wa kaburi, Joao Buino, wamekamatwa.

Ferreia alisema polisi wameshikilia sufuria mbili zilizokuwa na sehemu za mwili zilizopikwa za mtoto huyo aliyefukuliwa, ikiwa pamoja na mbavu, miguu na mikono. Foia pia alikuwa na mavazi na picha zilizoibiwa kutoka makaburini.

"Hizi ni dalili ambazo zinathibitisha ushiriki wa Rui Foia katika kufukua kaburi hilo", alisema.

Foia anaaminika kuwa ana ugonjwa wa akili, ambapo baadhi ya majirani zake katika kijiji cha Chimadzi wamelalamikia kuwa amezidisha matumizi ya bangi kwa kiasi kikubwa (Ingawa hakuna  ushahidi wa kisayansi kuwa aina hii ya dawa inaweza kusababisha ugonjwa wa akili). Wengine wanasema alikataa kutii maagizo kutoka kwa mganga wake ambayo yangemsaidia katika ugonjwa wake.

"Tunapaswa kuwasiliana na mamlaka ya afya", alisema Ferreira, "Ili waweze kutusaidia kutambua kama Foia kweli ana matatizo ya akili".

Ukiacha kaburi alilofukua Foia wiki mbili baada ya makaburi mengine 10 kugunduliwa yamefukuliwa, tisa yakiwa ya watoto wadogo na moja la mtu mzima nayo yalifanyiwa uhalifu katika makuburi ya kijiji cha Chimadzi.

Alikuwa akinywa pombe za asili katika nyumba ya mwanamke ambaye alimkaribisha nyama ambayo ilikuwa nayo katika sufiria. Mwanamke alipoona mkono na mbavu za mtoto katika sufuria aliogopa na kuomba msaada ili wamkamate Foia.

Umati wa watu walikusanyika na kutaka kumuua . Polisi walifika wakazuia jaribio hilo na kumpereka rumande.

MLA NYAMA ZA WATU AKAMATWA NA POLISI MLA NYAMA ZA WATU AKAMATWA NA POLISI Reviewed by By News Reporter on 2/05/2018 12:11:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.