Loading...
Msanii mkongwe wa filamu za kiHindi nyota Sridevi Kapoor amefariki dunia akiwa na miaka 54.
Mwigizaji huyo wa kike aliiaga dunia siku ya Jumamosi usiku baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo akiwa nchini Dubai, familia yake ilithibitisha.
Muigizaji huyo mkongwe na familia yake walikuwa Jumuia za nchi za kiarabu, Emirate kwa ajili ya sherehe ya ndoa, shemeji yake aliiambia mtandao wa Indian Express.
Na inaaminika walikuwa pamoja na mumewe, mtayarishaji wa filamu Boney Kapoor, na binti yake Khushi wakati alipofariki.
Sridevi alianza safari yake ya uigizaji akiwa na umri wa miaka 4, akiigiza katika filamu ya Thunaivan.
Aliionekana katika filamu za Bollywood akiwa na miaka 12 kitaka filamu iitwayo "Julie" na filamu yake ya mwisho kabla ya kuiaga dunia inakwenda kwa jina la MOM, iliyofanyika mwaka 2017.
Na mkongwe huyo ameacha majonzi mengi kwa waigazaji wakongwe katika tasnia ya filamu huko Bollywood India.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
SRIDEVI KAPOOR MKALI WA FILAMU ZA BOLLYWOOD AMEFARIKI DUNIA
Reviewed by By News Reporter
on
2/26/2018 11:24:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: