Loading...
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (SUGU) na Emmanuel Masonga, Katibu wa Kanda ya Nyasa Chadema, wamehukumiwa kwenda jela miezi mitano kwa kosa la uchochezi.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite, baada ya kujiridhisha kuwa watuhumiwa hao wana hatia dhidi ya kesi ya kutumia lugha ya fedheha kwa Rais John Magufuli
Sugu pamoja na Masonga walifikishwa mahakamani hapo kwa mara kwanza Januari 19, 2018, kwa kosa hilo walitoa kauli hizo katika mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana wakiwa viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Maneno yaliyomtia hatiani Sugu na mwenzake ni “Mhe Rais Magufuli hawezi kupendwa na watu kwa kumshoot risasi Lissu, kumtupa Jela miezi minne Lema, kumteka Ben saanane, kumteka Roma na kumzuia SUGU asiongee.”
Tuma neno 'SIASA' kwenda +255765112259 kupata habari za siasa punde zinapojiri.
SUGU, MASONGA WAHUKUMIWA MIEZI MITANO JELA
Reviewed by By News Reporter
on
2/26/2018 01:34:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: