Loading...
"Tafadhali naomba muukatae upumbavu huu, Mimi ni mzima na nina afya tele", muigizaji rambo akikataa uvumi unaondelea kuwa amefariki kwa kansa ya tezi dume.
Juzi Jumatatu jioni uvumi ulienea kwenye mitandao yote kwamba muigizaji nguli Sylvester Stallone (71) amefariki dunia kwa kansa.
Uvumi huo ulisambazwa mara kadhaa na watu katika kila kona ya mtandao kwamba amefariki dunia, pia ujumbe ulidai kwamba alifariki dunia kwa ugonjwa aliokuwa akiuficha wa kansa ya tezi dume.
Sylvester aliibuka na kukanusha uvumi huo kupitia mtandao wake wa Instagram na kusema: "Tafadhali muukatae ujinga huu... Ni mzima wa afya na mwenye furaha na bado naendelea na mapambano".
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
SYLVESTER STALLONE aka 'RAMBO' AKANUSHA UVUMI WA KIFO CHAKE
Reviewed by By News Reporter
on
2/21/2018 01:04:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: