Loading...

TAARIFA KWA UMMA: CHANJO YA SARATANI YA KIZAZI KUANZA KUTOLEWA RASMI APRILI 25

Loading...
Imetangazwa rasmi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kupitia ukarasa wake wa Facebook alisema:

"Leo nimefanya Mkutano wa Wadau wa Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV Vaccine). Serikali itaanza kutoa Chanjo hii kwa Wasichana wote wa umri wa miaka 9 - 14 ili kuwakinga na Saratani ya Mlango wa Kizazi.

Uzinduzi utafanywa na Mhe Makamu wa Rais, Mhe Samia Hassan Tarehe 25 April 2018, Dodoma. Mwaka huu 2018, tutaanza kuwachanja wasichana wa umri wa miaka 14...Tumelenga kuwafikia mabinti 616,734 kwa mwaka huu wa 2018.

Nitoe Wito kwa Wazazi/Walezi na Jamii kuhakikisha binti zetu wanapata chanjo hii ili kuboresha afya zao na kupunguza Vifo vitokanavyo na Saratani #HPV

Muhimu: #Chanjo ya #HPV itatolewa bila Malipo katika Vituo vyote vinavyotoa Huduma - Vya Serikali, Binafsi, Mashirika ya Dini. Kinga ni Bora kuliko Tiba."

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
TAARIFA KWA UMMA: CHANJO YA SARATANI YA KIZAZI KUANZA KUTOLEWA RASMI APRILI 25 TAARIFA KWA UMMA: CHANJO YA SARATANI YA KIZAZI KUANZA KUTOLEWA RASMI APRILI 25 Reviewed by By News Reporter on 2/27/2018 01:01:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.