Loading...

AMMWAGIA MUMEWE TINDIKALI SEHEMU ZA SIRI KISA WIVU WA MAPENZI

Loading...
Kwa mujibu wa mtandao mmoja huko Nigeria, mwanamke mmoja aliamua kummwagia mumewake tindikali sehemu za siri baada kugundua amempa ujauzito rafiki yake wa karibu. Mwanaume huyo alikimbizwa hospitali ya FMC Zaria katika jitihana za kunusuru maisha yake lakini alifia hospitalini hapo.

Stori ilikuwa hivi:
Mwanamke huyo mkatili alipata taarifa kwamba mumewake ana mahusiano ya siri na rafiki yake na tayari ameshampa ujauzito. Alifanya uchunguzi aligundua taarifa hizo ni za ukweli. Februari 15, 2018, wakati mumewake aliporudi kutoka kazini, mwanamke huyo alijifanya kama hana taarifa yoyote kama mumewake ana mahusiano ya siri na rafiki yake. Alimuandalia chakula na kuzungumza naye kirafiki kwa muda. Alimlaghai wakafanya mapenzi na baada ya tendo mwanaume alilala fofo. Mwanamke huyo alinunua tindikali ambayo ilikuwa kwenye betri ya gari ambayo aliifadhi chini ya uvungu wa kitanda tokea asubuhi na kuamua kummwagia sehemu zake za siri. Na mwanaume huyo alifikishwa hospitali kwa matibabu baada ya kuomba msaada kwa majirani lakini alifia hospitalini huko siku ya Jumanne, Februari 20, 2018.

Na polisi wa Kaduna walithibitisha mwanamke huyo yupo chini ya ulinzi na atafikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji na aliyemuuzia batri ya gari pia yupo chini ya ulinzi naye atafikishwa mahakamani kwa shtaka la kutekeleza njama za mauaji.

Mwanamke huyo alipohojiwa alisema: "Nampenda mumewangu sana, na sikuwa na kusudio la kumuua, nilichukizwa sana kusikia amempa ujauzito rafiki yangu wa karibu na hakuniambia. Naomba familia yangu, watoto wangu na serikali inisamehe."

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za gossip punde zinapojiri.
AMMWAGIA MUMEWE TINDIKALI SEHEMU ZA SIRI KISA WIVU WA MAPENZI AMMWAGIA MUMEWE TINDIKALI SEHEMU ZA SIRI KISA WIVU WA MAPENZI Reviewed by By News Reporter on 2/27/2018 01:49:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.