Loading...
Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Taifa, Humphrey Polrpole, amesema Chama Cha Mapinduzi, kimekataa maombi ya Mzee wa Monduli ya kuomba kurejea kutoka upinzani.
Amesema kwa sasa viwango vya mwanasiasa huyo, haviendani na kasi ya CCM ya wakati huu.
Aidha, Polepole amesema mzee huyo pamoja na wenzake waliohamia CHADEMA, akiwemo marehemu Kingunge Ngombare Mwiru, maisha yao yote yalikuwa CCM, hivyo waliondoka baada ya matarajio yao kutotimia.
Polepole aliyasema hayo jana, alipozungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Monduli, katika siku yake ya pili ya ziara yake ya kutembelea kaya zilizoweshwa na Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF).
Alisema anachokizungumza kuhusu mzee wa Monduli, kimetendeka hivi karibuni na Watanzania waliona.
Alisema kwa sasa mzee huyo hana ndani ya CCM hahitaji watu wanafiki, wenye kuleta migongano upya kati ya viongozi kwa viongozi na wanachama wenyewe.
Katibu huyo wa itikadi na Uenezi, alimtaka mzee huyo wa Monduli, kuendelea kubaki kwenye chama chake, ambako heshima imepotea kwa sababu amerudi kucheza siasa za mchangani.
Akimzungumzia marehemu Kingunge, alimuombea kwa Mungu apumzike kwa amani, ingawa alisikitishwa na kauli alizozitoa alipojiunga na CHADEMA kwamba CCM imeishiwa pumzi, hivyo haiwezi kuendelea kuongoza nchi.
"Unajua inaumiza sana, kauli eti CCM imeishiwa pumzi, haiwezi kuongoza nchi, unajua ni sawa na wewe upande Mlima Kilimanjaro, halafu ile hali ya kushindwa kupumua, ndivyo hivyo alivyomaanisha kwa CCM," alisema Polepole.
Alisema kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, alikutana na aliyekuwa mtumishi wa serikali miaka mingi iliyopita, ambaye kwa sasa umri umekwenda, akamwambia Mzee wa Monduli, alishawahi kukataliwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Sokoine, kujiunga kwenye chama kutokana na tabia yake.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za SIASA punde zinapojiri.
'TULIKATAA KUMPOKEA MZEE WA MONDULI' - HUMPHREY POLEPOLE
Reviewed by By News Reporter
on
2/28/2018 10:56:00 AM
Rating:
!['TULIKATAA KUMPOKEA MZEE WA MONDULI' - HUMPHREY POLEPOLE](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi_gT-K4Hrmxb9V_4tekKzAywpBR2VSKizNNupGBNktY0VxY44xMhB1gachTeRKRuFpi77E1BSXGEfX1fasKUWACRfANT3IBUz6CrkQAM8igQ9oJ9MfmFrmNVgE-YckyTy9MujobjZVcjBj/s72-c/polepole.jpg)
Hakuna maoni: