Loading...

UMEUMBWA KWA UPEKEE, ACHA KUJIFANANISHA NA WENGINE - Na Siri ya Utajiri

Loading...
Dr Maxwell Maltz aliwahi kuandika kwamba "Zaidi ya asilimia tisini na tano (95%) ya watu duniani hujihisi na kujiona wana mapungufu.  Mapungufu katika maisha yao, muonekano , uwezo ,maarifa , akili na mambo mengine kadhaa.

Tatizo hili limechangiwa kwa kiasi kikubwa na tabia ya kutumia muda mwingi kujilinganisha na watu wengine. Hili ni kosa kubwa ambalo watu wengi wamekuwa wakilifanya bila kujua madhara yake katika maisha yao.

Kila binadamu ameumbwa kwa upekee, wewe ni wewe na yule ni yule. Huna sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. Wewe si DHAIFU wala huna MAPUNGUFU  yoyote bali una vitu vya pekee tofauti na mwingine.

Usipime mafanikio yako kwa kujilinganisha na mwingine. Kipimo sahihi ni kulinganisha mafanikio yako na uwezo wako kwa muda husika. Jitahidi kutumia kila ulichonacho katika kiwango cha juu.

You Deserve The Best!
Vicent Stephen

Tuma neno 'MAKALA' kwenda +255765112259 kupata makala za siri ya utajiri.
UMEUMBWA KWA UPEKEE, ACHA KUJIFANANISHA NA WENGINE - Na Siri ya Utajiri UMEUMBWA KWA UPEKEE, ACHA KUJIFANANISHA NA WENGINE - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 2/24/2018 09:39:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.