Loading...
Taarifa rasmi kutoka nchini Libya zinasema angalau wahamiaji haramu 19 wamefariki dunia katika boti iliyozama karibu mji wa Bani Walid, uliopo kilometa 180 Kusini Mashariki mwa jiji la Tripoli.
Chifu wa hospitali ya Bani Walid, Mohamed el-Mabruk, aliitaarifu umma kuwa kuna watu 60 wengine walijeruhiwa wakati boti lilipopinduka mapema Jumatano.
Alisema zaidi ya wahamiaji 200, wengi wao wametokea Eritrea, Somalia na Sudan walikuwepo safarini. Ikiwa chanzo cha ajali hiyo hakikufahamika.
Libya iliingia katika machafuko kufuatia mapinduzi ya mwaka 2011 na sasa wamegawanyika kwa serikali ya upinzani na serikali kuu kwa upande wa mashariki na magharibi kila pande ikilindwa kwa maelfu ya wanamgambo.
Machafuko hayo yameifanya nchi ya Libya kuwa kituo cha kusafiria wahamiaji haramu kutoka Afrika na Mashariki ya kati wakitumaini kuwa watafika Ulaya.
WAHAMIAJI HARAMU 19 WAFARIKI KWA AJALI YA BOTI NCHINI LIBYA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
2/15/2018 11:44:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: