Loading...

WATU WASIOJULIKANA WAIBA RAMBI RAMBI KATIKA MAZISHI YA RADIO

Loading...
Msanii Mowzey Radio wa Uganda mwili wake ulipumzishwa tarehe 3 Februari, 2018 huko Nakawuka-kagga karibu na barabara ya Entebbe baada ya kufariki kwa majeraha ya ubongo ugomvi uliotoke katika baa ya De Bar.

Usiku kabla ya kwenda kuzikwa, Radio alipelekwa katika viwanja vya ndege vya Airstrip huko Kololo kwa ajili ya kuagwa mwili wake kwa mara ya mwisho na wasanii kadhaa walitumbuiza nyimbo zake kama kumkumbuka na boksi la rambi rambi liliwekwa karibu.

Balaam aliwekwa kama muangalizi wa boksi la rambi rambi, lakini siku chache baada ya Radio kuzikwa, boksi lilikutwa na pesa za Kiganda UGx 5 Milioni tu ndio zimebaki ndani ya boksi. Hakuna noti yeyote iliyobakizwa na wakati pesa zilijaa mpaka juu.

Familia ya Radio imesema hawajui nani aliyefungua boksi hilo lakini ni aibu kuona mtu anamuibia marehemu.

Ijue Whisky iliyosababisha kifo cha Mowzey Radio; kwa mujibu wa David Washington aliyekuwa karibu na msanii huyo siku ya tukio.

Alisema: "Radio alikunywa karibu nusu chupa ya whisky aina ya Johnnie Walker Red Label na ndipo alipokasirikiana na meneja wa baa ya 'De Bar' aliyewasili muda huo na kuperekea ugomvi mkubwa na hatimaye umauti ukamkuta."
WATU WASIOJULIKANA WAIBA RAMBI RAMBI KATIKA MAZISHI YA RADIO WATU WASIOJULIKANA WAIBA RAMBI RAMBI KATIKA MAZISHI YA RADIO Reviewed by By News Reporter on 2/10/2018 07:02:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.