Loading...

WATU WENGI NI MAGEREZA YA UWEZO WAO - Na Siri ya Utajiri

Loading...
Mtu anayeaminika duniani kuwa na akili nyingi na uwezo mkubwa inasemekana ametumia akili yake kwa kiwango cha asilimia kumi (10%) na asilimia tisini (90%) ya uwezo wake ikiwa bado haijatumika. Uwezo ambao hujatumika ndani yako ni mkubwa, mipaka yake haina kikomo.

Ulipoumbwa uliwekewa uwezo mkubwa sana ndani yako zaidi ya jinsi unavyofikiria. Badala ya kuruhusu kutumia uwezo huu wengi tumegeuka magereza ya kufunga uwezo wetu ulio ndani usitoke wala kutumika kubadilisha maisha yetu na ya wengine.

Aina yoyote ile ya maisha unayotaka iko ndani ya uwezo ulioufungia huko ndani. Hakuna sababu ya kulalamika maisha magumu huku kuna hazina ya uwezo wa kubadili maisha hayo umeifungia ndani yako.

Leo chagua jambo moja (LENGO) kisha fungulia uwezo uliofungwa ndani utumike kufanikisha hili. Usiogope, chukua jambo lolote unalolipenda kulifanya.

You Deserve The Best!
Vicent Stephen
WATU WENGI NI MAGEREZA YA UWEZO WAO - Na Siri ya Utajiri WATU WENGI NI MAGEREZA YA UWEZO WAO - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 2/12/2018 10:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.