Loading...

WIZ KHALIFA NA IZABELA WAACHANA RASMI

Loading...
Kulia Wiz Khalifa, kushoto Izabela.
Kufuatia habari zinazosema kwamba rappa Wiz Khalifa na mpenzi wake, Izabela Guedes hawapo tena katika mahusiano ya pamoja baada ya kufuta picha zao kila mmoja katika mitandao ya kijamii, imedaiwa kwamba rappa huyo alifanya usaliti kwa kutembea na mwanamitindo wa Kibrazili.

Chanzo karibu na wawili hao kiliiambia mtandao wa MediaTakeOut.com kwamba Izabela amemuacha Wiz kwa sababu aligundua alimsaliti na mpenzi wake wa zamani. Lakini wahusika walikataa kumtaja huyo mpenzi wake wa zamani aliyehusika.
Wiz Khalifa, Mwanae na Amber Rose aliyekuwa mke wake wa zamani.
Huyo mpenzi wake wa zamani hawezi akawa mkewe wa zamani na mama mtoto wake, Amber Rose, kwa sababu tayari anamuhusiano na rappa 21 Savage.

Wiz Khalifa na Izabela Guedes ambao walianza mahusiano yao mwaka 2016, walikuwa mfano wa kuigwa na wapendanao wengi kupitia mitandao ya kijamii.
WIZ KHALIFA NA IZABELA WAACHANA RASMI WIZ KHALIFA NA IZABELA WAACHANA RASMI Reviewed by By News Reporter on 2/14/2018 08:46:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.