Loading...

FURSA KWA UHIFADHI WA MTI WA MSANDALI - NEMC

Loading...
BARAZA la Taifa la Uhifadhi wa Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewataka Watanzania kujikita katika upandaji wa miti ya misandali kitaalamu ‘Osyris lanceolata’ ikiwa sehemu ya kutunza mazingira na pia fursa nzuri ya biashara kutokana na umuhimu wa miti hiyo katika kuzalisha bidhaa mbalimbali.

Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kutengenezea manukato cha Sierra limited kilichopo mkoani Manyara, Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC, Prof. Esnat Chaggu, alihimiza umuhimu wa kupanda wa msandali na aina mbalimbali ya miti ya mingine kutokana na faida zake kimazingira na kiuchumi.

“Hii ni fursa kwa vijana kujikita katika kupanda mashamba ya miti ya misandali ambayo faida yake kwa baadaye ni kubwa kutokana na uhitaji mkubwa wa mti huo katika kuzalisha malighafi ya kutengenezea manukato,” alisema Prof. Chaggu.

Alisema uwekezaji wa aina hii kwa vijana unawaletea faida kubwa kiuchumi baada ya kuivuna na pia mazingira yatakuwa yanaendelea kulindwa hali ambayo itapelekea ustawi wa nchi kimazingira kuimalika na pia kiuchumi.

“Ni muhimu kuhamasisha Watanzania nchini kupanda mti wa msandali na aina nyinginezo ambayo inafaida kubwa katika matumizi yake, kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendelea kuongeza idadi ya miti hii kuwa mingi nchini,” alisema Prof. Chaggu.

Prof. Chaggu alisema utafiti unaonyesha kupungua kwa mti huu kutokana na umuhimu wake mkubwa katika kutengeneza dawa za maradhi mbalimbali kwa binadamu na pia kutengeneza mafuta yanayotumika kuzalisha manukato

hivyo kama wadau wa mazingira wanalazimika kuhamasisha upandaji wa miti hii ili kuiendeleza na kuja kusaidia vizazi vijavyo.

“Nchi yetu ina maeneo mengi ambayo tunaweza kupanda miti ya aina ya msandali kwa lengo la kuongeza idadi ya miti hiyo nchini na pia kuwa sehemu ya fursa kwa vijana kujipatia kipato kupitia uwekezaji wa miti,” alisema.

Meneja wa Kiwanda cha Sierra, Ashish Upadhaye, alisema msandali una matumizi mengi hasa katika afya ya binadamu hivyo ni muhimu kama nchi kuweka kipaumbele katika kulinda miti ya aina hii na pia kuhamasisha upandaji wa miti hii ili iongezeke, hivyo italeta faida kubwa ikitumika kama malighafi ya kuzalisha bidhaa.

Mjumbe wa Bodi ya NEMC, Dk. Neduvoto Mollel, alisema faida za mti wa msandali ni nyingi hivyo wajibu wetu kama Baraza ni kusimamia zaidi katika uhifadhi wa miti ya aina hii kote nchini na pia kuhamasisha upandaji wa miti hii ili izidi kuongeza.
Na Saidi Mlanzi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FURSA KWA UHIFADHI WA MTI WA MSANDALI - NEMC FURSA KWA UHIFADHI WA MTI WA MSANDALI - NEMC Reviewed by By News Reporter on 5/22/2019 09:51:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.