Loading...

HUAWEI KUPATA PIGO, HIVI NDIVYO ITAKAVYOATHIRIKA AFRIKA!

Loading...
Bara la Afrika kuna takriban watu milioni 400 wanaotumia mtandao na kati ya hao kuna 60% wanatumia mfumo wa Android ambao ndio unatumikwa kwa simu kama za Huawei.

Ikiwa na soko lenye ukubwa wa takribani asilimia kumi na sita duniani, kampuni hiyo inatajwa kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa kubwa zaidi ya utengenezaji simu.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na hofu kutoka baadhi ya wadadisi kwamba huenda kampuni hiyo inatumiwa na Uchina kufanyia serikali za nje na pia wananchi wake ujasusi.

Lakini barani Afrika, kampuni hiyo pamoja na ile ya ZTE zimehusika sana katikaujenzi wa miundo mbinu nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda,miongoni mwa mataifa mengine.

Nchini Nigeria kwa mfano, Huawei ilishinda kandarasi ya dola milioni themanini kutengeneza mtandao wa dijitali wa simu wa GSM mnamo mwaka 2004.

Kwa kutathmini ukubwa wa uwepo wa kampuni hiyo Afrika wadadisi wanasema mzozo unaoshuhudiwa sasa inamaanisha kwamba biashara nyingi zitaathirika kutokana na changamoto ambazo Huawei inakumbana nazo.

Barrack Otieno moja ya wataalamu wa maswala ya sera za mtandaoni anaeleza kwamba, 'Waafrika wengi wanapokea mikopo midogo kupitia programu tumishi za simu ambazo zinatumia mfumo huo wa Android. Huenda sasa ikachangia watu wengi wakakosa mikopo na hivyo kuumia sana katika sekta za kibiashara'.

Huawei pia imezindua zaidi ya mitandao hamsini ya 3G, na kutengeneza mitandao ya huduma za zaidi ya serikali thelathini. Aidha kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika teknolojia zinazokua za 4G na 5G.
Na Vicky Daudi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
HUAWEI KUPATA PIGO, HIVI NDIVYO ITAKAVYOATHIRIKA AFRIKA! HUAWEI KUPATA PIGO, HIVI NDIVYO ITAKAVYOATHIRIKA AFRIKA! Reviewed by By News Reporter on 5/22/2019 09:29:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.