Loading...

WANAOPANDISHA BEI YA VYAKULA MWEZI MTUKUFU KUKIONA

Loading...
RAIS John Magufuli amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kutoa huduma za dini, ikiwemo elimu, afya na maji.

Aidha, ameagiza mamlaka husika kufuatilia wafanyabiashara wasipandishe bidhaa zinazotumiwa zaidi na Waislamu katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani unaoendelea.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana wakati wa Mashindano ya Kurani ya 20 ya Afrika, yaliyofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kushirikisha nchi 18 na washiriki 20.

Katika mashindano hayo, mshindi wa kwanza aliyenyakua kitita cha Sh milioni 20 na tiketi ya kwenda kufanya ibada ya hija ndogo (Umra) Makka nchini Saudi Arabia ni Mohammed Diallo (23) kutoka Senegal, na mshindi wa pili alikuwa ni Farouq Yakubu (21) kutoka Nigeria, aliyejinyakulia Sh milioni 15.

Mshindi wa tatu aliyenyakua Sh milioni 7.5 ni Shamsuddin Ally Hussein (21) kutoka Zanzibar huku Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM, Humphrey Polepole akimwongezea Sh milioni moja.

Rais Magufuli alimwongezea msichana huyo Sh milioni moja.

“Tutaendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kuliletea maendeleo taifa letu, hasa kutokana na kuisaidia serikali katika masula ya elimu, afya na maji,” alisema.

Aliipongeza Alhikma Foundation iliyoandaa mashindano hayo kwa kutoa elimu kwa Watanzania, kujenga misikiti na kuchimba visima.

Al-hikma inamiliki shule ya chekechea, shule ya msingi na shule mbili za sekondari; moja ya wasichana na nyingine ya wavulana.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAOPANDISHA BEI YA VYAKULA MWEZI MTUKUFU KUKIONA WANAOPANDISHA BEI YA VYAKULA MWEZI MTUKUFU KUKIONA Reviewed by By News Reporter on 5/20/2019 09:11:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.