Loading...

RAIS TRUMP AWACHIMBA MKWARA MZITO IRAN, 'WASIJARIBU ITAKUWA MWISHO WAO'

Loading...
Rais wa Marekani Donald Trump ameionya Iran kwamba itaharibiwa iwapo vita vitazuka katika ya mataifa hayo mawili.

''Iwapo Iran inataka kupigana , huo nduo utakuwa mwisho rasmi wa taifa hilo'' , alisema katika jumbe wa Twitter siku ya Jumapili. ''Musijaribu kuitisha Marekani tena''.

Marekani imepeleka meli zaidi za kivita na ndege katika eneo la mashariki ya kati katika siku za hivi karibuni.

Ujumbe huo wa Twitter wa bwana Trump unaadhimisha kubadilika kwa msimamo baada ya jaribio la hivi karibuni la la kuficha uwezekano wa vita kati ya mataifa hayo mawili.

Siku chache zilizopita , rais huyo aliwaambia washauri wake kwamba hapendelei shinikizo ya Marekani dhidi ya Iran kubadilika na kuwa vita.

Na alipoulizwa na waandishi wa habari siku ya Alhamisi iliopita iwapo Marekani ilikuwa ikijiandaa kivita , bwana Trump alijibu: Sidhani.

Iran pia imepinga madai ya kuwepo kwa hali ya wasiwasi. Siku ya Jumamosi waziri wa maswala ya kigeni wa taifa hilo Javad Zarif alisema kuwa hakuna hamu ya Vita.

''Hakutakuwa na vita kwa kuwa hatutaki vita na hakuna mtu ambaye anafikiria kuivamia Iran katika eneo hili'', Mohammed Javad Zarrif aliambia chombo cha habari cha Iran.
Na Frank Kavikule.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS TRUMP AWACHIMBA MKWARA MZITO IRAN, 'WASIJARIBU ITAKUWA MWISHO WAO' RAIS TRUMP AWACHIMBA MKWARA MZITO IRAN, 'WASIJARIBU ITAKUWA MWISHO WAO' Reviewed by By News Reporter on 5/20/2019 08:56:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.