Loading...

JUISI INASABABISHA KIFO CHA HARAKA - TAFITI

Loading...
Utafiti unaonyesha matumizi ya juisi kwa wingi yanapunguza miaka ya kuishi humu duniani. 

Kulingana na utafiti huo uliofanywa na watafiti wa matibabu kutoka Marekani, glasi moja ya juisi yenye kipimo cha mililita 354 kwa siku inaongeza uwezekano wa kufariki mapema kwa asilimia 24.

Hii ni kinyume namatumizi ya vinywaji vingine kama soda kwani uwezekano wa kufa mapema ukitumia soda mililita 340 kwa siku uko katika hatari ya kuondoka duniani mapema kwa asilimia 6 tu.

Mtafiti Kate Patton aliiambia Philadelphia CBS kuwa kiwango ambacho mtu anakunywa ni muhimu sana kwenye utafiti huo.

“Ningetaka wagonjwa wangu wasikunywe zaidi ya mililita 236 ya juisi kwa siku. Kiwango sawa kabisa ni mililita 115 pekee,” Patton alisema.

Watafiti hao walisema kipimo cha juu kina madini ya juu ya fructose ambayo huongeza kiwango cha homoni mwili kutofautiana na insulin.

Hali hiyo hufanya mafuta kuongezeka mwili na hivyo kusababisha matatizo ya moyo na pia ugonjwa wa kisukari.
Na Bakari Juma.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JUISI INASABABISHA KIFO CHA HARAKA - TAFITI JUISI INASABABISHA KIFO CHA HARAKA - TAFITI Reviewed by By News Reporter on 5/20/2019 08:44:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.