Loading...

BENIN YACHUNGUZA NAMNA WATALII WAWILI WA UFARANSA WALIVYOTEKWA

Loading...
Serikali ya Benin imesema imeanza kuchunguza kutekwa kwa watalii wawili, raia wa Ufaransa waliotekwa na watu wenye silaha tarehe 1 mwezi wa Mei na kupelekwa nchini Burkina Faso.

Licha ya kutekwa, watalii hao Patrick Picque na Laurent Lassimouillas waliokolewa baada ya operesheni kuongozwa na wanajeshi wa Ufaransa.

Operesheni hiyo ilisababisha wanajeshi wawili kupoteza maisha.

Siku ya Jumanne, rais Emmanuel Macron aliongoza mazishi ya wanajeshi hao wawili na kuwaita mashujaa wa taifa hilo.

“ Cédric de Pierrepont naye Alain Bertoncello, wamekufa ni wazi kuwa kazi iliyofanyika ilipata mafanikio makubwa, lakini ona tumewapoteza wanajeshi wetu wawili, nao wamekufa kama mashujaa kwa ajili ya taifa la Ufaransa,” alisema rais Macron.

“Wamekufa kama mashujaa kwa sababu waliona hakuna kilicho na  thamani kubwa kuliko maisha ya wananchi waliokuwa wametekwa,” aliongeza.

Nchi ya Burkina Faso imeendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama, kutokana na kuwepo kwa makundi yenye silaha ambayo yameendelea kupambana na vikosi vya usalama.
Na Mohamedi Makame.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BENIN YACHUNGUZA NAMNA WATALII WAWILI WA UFARANSA WALIVYOTEKWA BENIN YACHUNGUZA NAMNA WATALII WAWILI WA UFARANSA WALIVYOTEKWA Reviewed by By News Reporter on 5/18/2019 10:02:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.