Loading...

UTATA WA KIDOPLOMASIA KATI YA KENYA NA UAE WAPAMBA MOTO

Loading...
Utata wa kidiplomasia kati ya Kenya na falme za kiarabu unazidi kupamba moto baada mzozo kuhusu biashara ya dhahabu.

Tayari UAE imeiandikia Kenya barua ikitaka raiya wake alipwe takriban shilingi bilioni nne ambazo inasema alipoteza kwenye sakata ya biashara hiyo iliyowashirikisha wanasiasa wa Kenya sawa na wafanyibiashara matapeli.

UAE inataka Ali Zandi, ambaye anamiliki kampuni ya biashara ya dhahabu ya Zlivia kulipwa fedha hizo. Zandi ndugu na mwanafamilia wa mfalme wa Dubai.

Huku tayari akiwa amechimba mkwara mzito na kusema: "Wapendwa Kenya nimewapa masaa 24 ili mnipatie dhahabu zangu. La sivyo nitakuja kuzichukua huko mwenyewe, na nitakapo fanya hivyo basi nitawageuza nta."

Masaibu yalianza wakati ambapo Zandi aliingia kwenye mkataba na mfanyibiashara wa Kenya Zaheer Jhanda akitaka amsaidie kusafirisha tani kadhaa za dhahabu kutoka nchini Congo mpaka Dubai.

Baada ya kuskizana, shughuli hizo zilianza lakini utata ukaibuka baada ya Zandi kupata ripoti kuwa dhahabu zake zilikuwa zimezuiliwa kwenye uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Hapo ndipo inadaiwa alianza kutuma mamilioni ya pesa kwa baadhi ya wanasiasa na wafanyibiashara hao ili kumsaidia kuhakikisha mzigo wake unawachiliwa. 

Hata hivyo, Jhanda, akiongea na gazeti la Standard Jumapili, Mei 19, alikanusha madai hayo akisema kuwa hakuna dhahabu iliyokuwa imeingia humu nchini.

“Kampuni hiyo ilinipa kazi ya kuwashauri kuhusiana na ulipaji wa ushuru pamoja na kusafirisha dhahabu kutoka nchi ya Kidemokrasia ya Congo mpaka humu nchini,” alisema.

“Dhahabu ya shilingi bilioni 30 haiwezi kuwa humu nchini na serikali iwe haina taarifa,” aliongeza. 

Jhanda, 40, aliongeza kuwa anamiliki asilimia 12 ya kampuni ya Zlivia inayofanya biashara ya dhahabu na kumilikiwa na Zandi. 

Seneta Moses Wetangula, Kiongozi wa ODM na Rais Uhuru Kenyatta pia wametajwa kwenye sakati hiyo. 

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i vile vile alijipata kwenye sakata hiyo huku mhusika mmoja akisema ndiye alidai hongo ili mzigo uliokuwa umezuiliwa kuwachiliwa. 

Hata hivyo, kiongozi wa mshataka ya umma Noordin Haji siku ya Jumamosi, Mei 19, alitaka uchunguzi kabambe kufanywa kuhusiana na sakata hiyo.
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UTATA WA KIDOPLOMASIA KATI YA KENYA NA UAE WAPAMBA MOTO UTATA WA KIDOPLOMASIA KATI YA KENYA NA UAE WAPAMBA MOTO Reviewed by By News Reporter on 5/22/2019 10:27:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.