Loading...

DIAMOND NA ZARI WAACHANA SIKU YA VALENTINE

Loading...
Jana siku ya wapendanao Zari the Boss Lady aliyekuwa mpenzi wake msanii Diamond Platinumz ameachana na nyota wa mziki wa bongo fleva Tanzania kwa kuandika ujumbe kupitia mtandao wake wa Instagram.

Aliandika ujumbe huo na kusema: "Nafahamu kwamba ni vigumu sana kufanya maamuzi kwa hili. Kunatetesi nyingi kupitia zilizozagaa katika mitandao lakini zingine zikiwa na ushahidi au ukweli ndani yake kwamba Diamond Platinumz ameendelea kunisaliti and kwa machungu nimeamua kuacha na Diamond ili HESHIMA, UTU na UIMARA wangu usiathiriwe.
Tunaachana kama wapenzi ila tutaendelea kama wazazi wenza."

"Na hii haitanifanya nisiwe mtafutaji, na kama mama mlezi na bosi wa kike ambavyo mnijuavyo.
Nitaendelea kutengeneza taswira yangu kwa kuwapa hamasa wanawake wenzangu kuwa mabosi wakike pia.
Nitawafundisha watoto wangu wa kiume siku zote wajifunze kuwaheshimu wanawake, na mtoto wangu wa kike nini maana ya kujiheshimu."

Chini ni picha ya ushahidi ya ujumbe huo:

DIAMOND NA ZARI WAACHANA SIKU YA VALENTINE DIAMOND NA ZARI WAACHANA SIKU YA VALENTINE Reviewed by By News Reporter on 2/15/2018 10:40:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.