Loading...

ZUMA, MTU ALIYEFANYA MENGI BILA ELIMU YA DARASANI

Loading...
Jacob Zuma ni Rais wa aina yake na mwenye utata kuwahi kutokea Afrika Kusini baada ya utawala wa weupe mwaka 1994. Amekuwa ni mwanasiasa mwenye maisha tisa akiponea chupuchup kashfa kadhaaa ambazo zineweza kuangamiza kabisha nafasi na historia ya kisiasa ya mtu mwingine yeyote.
Lakini Zuma aliyezaliwa katika familia masikini na baadae kusihi uhamishoni sababu ya kupinga ubaguzi wa rangi kabla ya kupanda ngazi na kushika hatamu kama rais wa watu, hawezi kunusurika kashfa hizi kila mara.
Muula wake wa pili na wa mwisho unafikia ukomo ,siyo kiongozi tena wa chama tawala ANC (African National Congress) licha ya kukana mara zote tuhuma za rushwa dhidi yake tuhuma hizo zimekuwa zikijirudia kila mara.
Itakuwa si jambo la busara kumfuta sasa wakati mapema kabla ya hata kuingia madarakani Zuma tayari alikuwa anatuhuma kadhaa.
Urais wa Zuma ulitiliwa mashaka hata kabla ya kuingia madarakani, mwaka 2009 kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huo tayari zuma alikuwa akikabiliwa na tuhuma za rushwa na ubakaji.
Alituhumiwa kumbaka rafiki wa familia yake ambaye anaishi na virusi vya ukimwi mwaka 2006, lakini licha ya ushaidi Zuma aliambia mahakama kuwa alioga ili kujikinga na kupata virusi vya ukimwi ambavyo vinge muandama muda wote wa uraisi wake.
Tuhuma za rushwa dhidi yake hazikupotea kirahisi hata baada ya kutupiliwa mbali kiutata na tume ya mwendesha mashtaka wa serikali juma moja kabla ya uchaguzi ulio muweka madarakani
Lakini tuhuma za utakatishaji wa fedha na kupanga mpango katika mkataba tata wa silaha wa mwaka 1999 bado zina muandama, kwani mwaka 2017 mahakama ya upeo nchini humo iliamua tuhuma 18 za rushwa dhidi yake zita rejewa.
Mara zote Zuma amekanusha tuhuma hizo na kuapa kuachia ngazi ikithibitika kama ni kweli amehusika.

'Raisi wa Watu'
Ulikuwa ni utu wake ndio ulimpeleka Zuma madarakani mwaka 2009 wafuasi wake waliona namna alivyokuwa akikubalika na wengi na kushika hisia zao na kuwa mbadala wa Rais Thabo Mbeki ambaye alionekana kuwa mbali na watu.
''Ni mtu anayesikiliza, hajifanyi kuwa mungu mtu ''alisema mfuasi wake mmoja ambaye jina lake halikufahamika wakati Bw Mbeki alipokuwa anaelekea kuanguka huku wafuasi wake wakielezwa kuongoza mapambano ya kumuweka Zuma madarakani baada ya kunyakua uongozi wa chama caha ANC mwaka 2007.
Ukaribu wa bwana Zuma usimamizi na utetezi wa mila na desturi katika familia ni miongoni mwa sababu zilizo pelekea kujizolea wafuasi hasa kwa raia masikini wengi wao wakiwa ni wakazi wa vijijini.
Zuma mwenye miaka 75 anajivunia ndoa za mitara kama ilivyo desturi ya wazulu Zuma kwa sasa ana wake wa nne ameoa mara sita ana watoto 21 na mmoja wa wake zake raia wa Msumbiji Kate Mantsho alijiua mwaka 2000.
Kadhalika anasifa ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa zake na analea mtoto wa nje ya ndoa na mwanamke mwingine.
Imani hii ya Raia kwa Zuma kama rais wa watu haikudumu kwa muda mrefu ,mapema mwaka 2013 moshi ulianza kufuka baada ya Zuma kuboresha makazi yake ya kijijini kwao Nkandla kaskazini mwa KwaZulu-Natal akitumia hela za serikali.
Wakati wa ibada ya mazishi ya Rais wa kwanza mweusi wa Taifa hilo Nelson Mandela wafuasi wa ANC walikuwa wakimkosoa wazi wazi mbele ya wageni mbali mbali wa kimataifa akiwemo aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo Barrack Obama.
''Anakula wakati tuna njaa'' mmoja wa waandamanaji alisema na kuamsha hasira kwa waandamanaji juu wa maboresho zuma aliyofanya kwenye makazi yake huko Nkandla ikiwa na eneo la kufugia ng'ombe, ukumbi wa Sanaa , bwawa la kuogelea ,sehemu ya wageni na banda la kuku.
Bw Zuma alifanikiwa kulipa hela za ziada alizotumia.

Visa vya kisheria vinavyomuandama Zuma

  • 2005: Alituhumiwa kwa rushwa ya mabilioni ya dola kwenye mkataba wa silaha wa mwaka 1999 madai ambayo yalitupiliwa mbali kabla hajawa rais mwaka 2009
  • 2016: Mahakama iliamuru ashitakiwe kwa makosa 18 ya rushwa dhiya ya mkataba wa silaha ambao alikatia rufaa
  • 2005: Aishitakiwa kwa kumb'aka rafiki wa familia na kufutiwa mashitaka 2006
  • 2016: Mahakama iliamuru kuwa amekiuka kiapo chake kama raisi na kutumia fedha za serikali kuboresha makazi yake binafsi fedha ambazo alizilipa baadae
  • 2017: Wakili wa serikali alisema atateua jaji kiongozio wa kamati ya kuchunguza iwapo ana uhusiano na familia tajiri ya Gupta madai ambayo ameyakanusha
  • 2018: Zuma alikubali maombi hayo

Miaka mitatu Mahakama kuu nchi ya Afrika kusini iliamua kwamba amekiuka katiba kwa kushindwa kulipa pesa za serikali alizo tumia kuboresha makazi yake binafsi
Rasi Zuma aliwaomba radhi raia wa nchi hiyo kwa tuhuma hizo na kulipa fedha hizo.
Lakini tuhuma hizi za makazi zilitarajiwa kufunikwa na tuhuma kubwa zaidi za namna alivyoingia madarakani.
Baada ya muda kidogo mahusiano ya Zuma na familia tajiri ya India Gupta yakaanza kumulikwa tuhuma zikiwa ni kwamba walishinikiza uteuzi wa baraza la mawaziri ili waweze kupata mikataba yenye fedha nyingi ya serikali.
Tuhuma hizi zimepingwa vikali na Zuma mwenyewe na hata familia ya Gupta.
Akiwa na miaka 17 Zuma alijiunga na ANC na kuwa mwanachama hodari katika tawi lake la Jeshini Umkhonto We Sizwe, in 1962.

Wake zake Zuma

  • Gertrude Sizakele Khumalo alimuoa mwaka 1973
  • Nompumelelo Ntuli (2008)
  • Thobeka Madiba (2010)
  • Gloria Bongi Ngema (2012)

Wake aliotalikiana nao

  • Nkosazana Dlamini-Zuma (alimuoa mwaka 1972; na kuachana naye 1998)
  • Kate Mantsho (alimuoa 1976; alifariki 2000)
Alihukumiwa kwa kula njama za kutaka kupindua serikali ya kibaguzi ya makaburu na kufungwa miaka 10 katika gereza la watu hatari zaidi katika kisiwa cha Robben pamoja na Nelson Mandela.
Inaelezwa Zuma alikuwa akichochoa morali ya wapigania uhuru hawa kwa nyimbo na tungo za kizalendo na wengi wana amini hiki ndo kilimfanya kuwa maarufu miongoni mwa Raia hata wale wa vijijini kabla ya kuupata uraisi
Chini ya utawala wa Zuma uchumi umekuwa ukiyumba na idadi ya wasio kuwa na ajira imeongezeka kwa asilimia 28 huku kukiwa na maandamano ya mara kwa mara watu wakidai maisha bora.
Ni wazi kwamba yapo Zuma aliyoshinda kama Rais zuma ameshinda kukosolewa na harakati baada ya kutangaza sera ya Ukimwi ya taifa hilo mwaka 2010 na hili limepunguza kwa kiwango kikubwa vifo vya waathirika wa Ukimwi kwa kuwapatia dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo ARV.
Afrika ya kusini ina wastani wa watu millioni tano wanaoishi na virusi vya ukimwi ikiwa ni kiwango cha juu kuliko taifa lolote.

Kuzomewa

Ni kweli kwamba Julius Malema na chama chake cha Economic Freedom Fighters (EFF) wamekuwa nyuma ya majaribio kadhaa ya kutaka kumtoa madarakani Rais Zuma

Elimu yake

Zuma licha ya kufanya mengi makubwa na kuongoza kwa muda mrefu madarakani lakini hakuwai kupata elimu ya darasani, baada ya baba yake mzazi kufariki akiwa na umri wa miaka minne (4) aliamua kufanya vibarua mitaani ili alishe familia yao na kupata pesa yakuweza kumpa elimu ya kusoma na kuandika tu. Na alipoweza kusema alijifunza mwenye kwa kusoma riwaya za mtunzi Shakespere na hata kujua mengi zaidi katika siasa na uongozi ki ujumla.
ZUMA, MTU ALIYEFANYA MENGI BILA ELIMU YA DARASANI ZUMA, MTU ALIYEFANYA MENGI BILA ELIMU YA DARASANI Reviewed by By News Reporter on 2/16/2018 11:49:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.