Loading...
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Godfrey Katusiime (50), mkazi wa Kata ya Bwikya, wilaya ya Hoima, Uganda amekamatwa na polisi kwa kosa la kutekeleza utekaji nyara bandia.
Kwa mujibu wa polisi, wakati Katusiime akitoweka nyumbani kwake siku ya Alhamisi, alimpigia simu mkewake aliyetambulika kwa jina la Alice Nyandera akidai kwamba ametekwa nyara. Akiripoti madai hayo kwamba watekaji nyara walihitaji fidia ya pesa za Kiganda Shs. 2 milioni ili wamuachie huru la sivyo wangemuua.
Katusiime alienda mbali zaidi akisema na watekaji hao wametoa masaa sita (6) tu, ili wakabidhiwe pesa hizo. Hii iliwafanya wahusika wafamilia walianza kutafuta pesa huku na kule ili wamtumie Katusiime kwenye simu yake ya mkononi.
Hata hivyo, polisi walipofanya uchunguzi wao ndipo walipogundua Katusiime ndio aliyepanga utekaji nyara huo bandia na wakamkamata na kuokoa kiasi cha pesa ambacho alibaki nacho baada ya kutumia kiasi cha Shs. 500,000. Na alipobanwa na polisi akasema alitaka pesa hizo ili akalipe deni alilokuwa akidaiwa na Encot Microfinance huko Hoima.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
ADANGANYA 'KUTEKWA NYARA' KISA UGUMU WA MAISHA
Reviewed by By News Reporter
on
3/09/2018 11:38:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: