Loading...

AJARIBU KUJIUA KWA KUJIRUSHA KATIKA NDEGE - VIWANJA VYA NDEGE VYA NTEBBE, UGANDA

Loading...
Mmoja wa wafanyakazi katika ndege ambayo ilipaswa kuruka katika Viwanja vya Ndege vya Kimataifa vya Ntebbe alifungua mlango wa dharula na kujirusha nje ya ndege na kupatwa na majeraha makubwa.

Ndege hiyo ya shirika la Emirates - EK 730 ambayo iliwashusha abiria mjini Entebbe na ilikuwa ikijiandaa kuwapakiza abiria wengine wanaolekea Dubai wakati wa tukio hilo likitokea siku ya Jumatano mchana, kilisema chanzo kimoja hapo uwanja wa ndege.

Mfanyakazi huyo, ambaye alifahamika kwa haraka, alifikishwa hospitalini haraka kwa ajili ya huduma ya kwanza na matibabu zaidi.

Chanzo hasa cha tukio akiweza kugundulika lakini baadhi ya mashahidi waliona kama ni jaribio la kujiua. Alionekana kushikilia chupa ya glasi kabla ya kujirusha chini.
Mashuhuda wengine walisema walimuona katika majibizano na mwenzake. Baada kujirusha alivunjika miguu na sehemu za mwili wake kukatwa na vipande vya chupa vilivyovunjika kwenye chupa aliyokuwa ameshikilia.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
AJARIBU KUJIUA KWA KUJIRUSHA KATIKA NDEGE - VIWANJA VYA NDEGE VYA NTEBBE, UGANDA AJARIBU KUJIUA KWA KUJIRUSHA KATIKA NDEGE - VIWANJA VYA NDEGE VYA NTEBBE, UGANDA Reviewed by By News Reporter on 3/15/2018 11:48:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.