Loading...

AMBER ROSE AJIFUTA MTANDAONI KISA MWANAE KUITWA SHOGA

Loading...
 Amber Rose ambaye mwenye wafuasi zaidi ya milioni 16.8 katika mtandao wa Instagram aliamua kufuta picha zake zote na kujitoa urafiki na kila mtu aliyekuwa amejiunga naye urafiki.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya mwanae wa kiume, Sebastian, 5 kudhalilishwa kwa kuitwa shoga kwa kupenda nyimbo za mwanamuziki Taylor Swift.

Yote yaliibuka baada ya Amber Rose kupandisha video siku ya Jumanne, ambayo ilimuonyesha mtoto wake huyo wa kiume, Sebastian akifungua boksi kama zawadi kwa mwanamuziki nyota Taylor Swift, ambalo lilikuwa na tiketi mbili za Ziara yake ya Revange World.

Lakini mtandao ulivamia ukurasa wake wa Instagram ana kuanza kumshambulia kwa kumdhalilisha mwanae na kumuita 'Shoga' kwa kumkubali nyota huyo.

Siku ya Ijumaa, Amber Rose aliamua kufuta kila kitu kwenye ukurasa wake wa Instagram ili asipate udhalilishaji mwingine. Tazama ushahidi wa picha hapa chini...
Na Neema Joshua.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
AMBER ROSE AJIFUTA MTANDAONI KISA MWANAE KUITWA SHOGA AMBER ROSE AJIFUTA MTANDAONI KISA MWANAE KUITWA SHOGA Reviewed by By News Reporter on 3/26/2018 01:30:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.