Loading...

MAENEO BORA YA KUTEMBELEA KUSINI MWA SUDANI

Loading...
Wau ni Mahali ambapo hujumuisha makabila kadhaa ya Kisudani, imetawaliwa na ardhi yenye rutuba, hali ya hewa nzuri na maeneo mengi ya utalii.
Hifadhi ya Taifa ya Boma ni sehemu ambayo utapata kuona wanyama mbali mbali kama vivutio katika mbuga hiyo. Na watu wengi huifananisha na Hifadhi ya Serengeti kutokana na wanyama kwa na mtindo wa kuhama kwa pamoja kutoka eneo moja hadi jingine.

Ndani ya hifadhi kunapatikana wanyama kama Pundamilia, Chui, Pofu na mandhari nzuri za kuvutia.
Hifadhi ya Taifa ya Southern ni mahali inayochukua karibu kilometa za mraba 7800 katika ardhi muhimu ya nchi ya Sudani Kusini na ndio hifadhi inayotunzwa sana kuliko zote nchini humo.

Ndani yake kuna wanyama kama Simba wa Kongo, Tumbili, Vinyonga na wengine wengi.
Hifadhi ya wanyama ya Kidepo ipo upande wa kusini zaidi mwa Sudani ya Kusini.

Ni hifadhi yenye mahali pazuri pakupumzikia ambapo itamfanya mtalii ajisikie mwenye furaha. Ni mbuga yenye uoto wa asili wa nyasi nyingi na zenye ustawi mzuri na kuwapatia wanyama katika hifadhi malisho ya kutosheleza.
Juba ni wa kihistoria ambao ndio inapatikana kona ya mto Nile na uligundulika mwaka 1922 na Wajerumani ndipo walipoamua kujenga daraja kubwa lililounganisha pande mbili za mji huo mpaka leo. Mji huu unamzunguko mkubwa biashara na watalii wanaoingia na kutoka kutokana na historia yake.
Malakal ni mji wenye uwanja wake wa ndege na upo karibu na mto Nile Nyeupe na kuifanya kuwa mji wa kupendeza zaidi ukilinganisha miji mingine. Mji huu pia una mbuga kama Ez Zeraf katika upande wake wa mashariki.
Na Geofrey Okechi.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za utalii punde zinapojiri.
MAENEO BORA YA KUTEMBELEA KUSINI MWA SUDANI MAENEO BORA YA KUTEMBELEA KUSINI MWA SUDANI Reviewed by By News Reporter on 3/26/2018 12:26:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.