Loading...

AMZAWADIA MKE WAKE FIGO SIKU YA KUMBU KUMBU YA NDOA YAO

Loading...
Mume aliyekuwa akifurahia miaka 23 ya ndoa ameamua kumpatia mke wake figo yake moja kama zawadi ya kuokoa maisha yake. 

Bwana aliyejulikana kwa jina la Cesar Calle alimpatia zawadi hiyo mkewake ambaye alikuwa akisumbuliwa maradhi ya figo mlongo mzima.

Wawili hao walizungumza kuhusiana na upasuaji wa masaa matano wakati wa mkutano wa hadhara katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mkoa huko Hollywood, Marekani, ambapo operesheni ilifanyika mwezi Februari 19. "Nilihisi kama nimegewa mamilioni ya dola," Monica alisema, wiki tatu baada ya upandikizi.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Sun Sentinel, Cesar alisema, "Mimi kufanya hivi, ni kitu kikubwa. Nilishtushwa. Nilifikiri kwamba haitowezekana."

Kwa sasa Monica anaendelea vizuri na wako na furaha katika maisha yao.
Na Fatma Pembe.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za afya punde zinapojiri.
AMZAWADIA MKE WAKE FIGO SIKU YA KUMBU KUMBU YA NDOA YAO AMZAWADIA MKE WAKE FIGO SIKU YA KUMBU KUMBU YA NDOA YAO Reviewed by By News Reporter on 3/19/2018 07:54:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.