Loading...

BIASHARA YA NYAMA YA NYANI INANIZALISHIA HADI MILIONI 2 KWA WIKI - MAMA ELOFA, KONGO

Loading...
Nyama ya kobe, Nyoka na Nyani ni chakula maarufu kwa jamii za watu wa Jamhuri ya Kongo. Ambapo inaweza ikawa inashangaza katika jamii za Afrika Mashariki, lakini Wakongo wamechunguza sana nyama pori za namna hiyo na hatimaye kuwa sehemu ya chakula chao maarufu.

Ingawa mnamo mwaka 2014, iliwagharimu vifo vya watu 49, baada ya wawindaji huko Jeera, walioko umbali wa kilometa 1000 kaskazini mwa Kinshasa walipomuua nyani na kumla kama chakula cha usiku. Siku moja baadae, mkewe na watoto walifariki wote. Ulipofanyika uchunguzi kwa kina ndipo ulipogundulika ugonjwa wa Ebola.

Baada ya hapo Wakongo wengi walipatwa na hofu juu ya nyama ya nyani lakini wengine waliendelea kula kwa kile walichodai kuwa ni tamu ukilinganisha na nyama nyingine.

Nyama hizo za nyani na wanyama wengine kutoka porini zinauzwa Tshs. 30,000  kwa kilo hadi 65 elfu kwa makadirio ya juu.

Mama mmoja mfanya biashara wa nyama za nyani aliyejukana kwa jina la Mama Elofa amedai biashara hiyo inamtengenezea pesa nyingi hasa siku za mwisho wa juma, ambapo anaweza kukusanya hadi milioni 2 pesa za Kitanzania kwa wiki.

"Kutokana na wapenzi wa nyama ya nyani kuongezeka kwa wingi, wataalam wa maswala ya wametushauri kuikaanga nyama hiyo kwanza kabla ya kuiuza ili kuuwa virusi vya ugonjwa wa Ebola ila kuwahakikishia usalama wateja", alisema mama Elofa.

Wakongo ni walaji wa kubwa wa nyama ya nyani, na wanaiita "Makaka" kwa Kikongo, ijapokuwa kuna tafiti zinaonyesha virusi vya ugonjwa upendelea kukaa katika nyama hiyo.
Na Neema Joshua.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kijamii punde zinapojiri.
BIASHARA YA NYAMA YA NYANI INANIZALISHIA HADI MILIONI 2 KWA WIKI - MAMA ELOFA, KONGO BIASHARA YA NYAMA YA NYANI INANIZALISHIA HADI MILIONI 2 KWA WIKI - MAMA ELOFA, KONGO Reviewed by By News Reporter on 3/28/2018 12:09:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.