Loading...

FORBES: TRUMP ASHUKA ORODHA YA MATAJIRI DUNIANI 2018

Loading...
Rais wa Marekani Donald Trump ameshuka nafasi 222 katika orodha ya kila mwaka ya watu tajiri zaidi duniani ambayo hutolewa na jarida la Forbes.

Mali yake imeshuka thamani kutoka $3.5bn (£2.5bn) hadi $3.1bn.

Jarida hilo limesema kushuka kwa utajiri wa Trump kumetokana zaidi na kushuka kwa thamani ya nyumba na vipande vya ardhi New York na pia kushuka kwa mapato kutoka kwa viwanja vyake vya kuchezewa mchezo wa gofu.
Anayeongoza orodha ya matajiri wa kupindukia ni mmiliki wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos.

Utajiri wa Bezos umepanda na kufikia $112bn kutoka takriban $39.2bn mwaka jana.

Kuimarika kwa utajiri wa Bw Bezos ndiko kwa juu zaidi katika historia.

Amemuondoa mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates kutoka uongozini kwenye orodha hiyo.

Utajiri wa Gates unakadiriwa kuwa $90bn mwaka huu kutoka $86bn, na ndiye anayeshikilia nafasi ya pili.

Bw Gates ameongoza orodha hiyo kwa miaka 18 kati ya miaka 24 iliyopita.

Forbes wanasema kuna mabilionea 2,208 (kwa kutumia dola za Marekani) ambao walishirikishwa katika orodha ya 32 ya kila mwaka ya jarida hilo.

Matajiri hao kwa pamoja wana utajiri wa $9.1 milioni.

Miongoni mwao, kuna mabilionea 259 wapya ambao walijipatia utajiri wao kutoka katika biashara za aina nyingi zikiwemo nguo za harusi, wanasesere wa kuchezewa na watoto na magari yanayotumia umeme.

Mwekezaji mmarekani Warren Buffett ndiye wa tatu utajiri wake ukiwa $84bn. Utajiri wake umepanda kutoka $75.6bn mwaka uliotangulia.

mtu tajiri zaidi Ulaya ndiye wa nne kwenye orodha hiyo, ambaye ni mmiliki wa kampuni ya bidhaa za kifahari ya LVMH, Bernard Arnault, ambaye utajiri wake ni $72bn.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za biashara punde zinapojiri.
FORBES: TRUMP ASHUKA ORODHA YA MATAJIRI DUNIANI 2018 FORBES: TRUMP ASHUKA ORODHA YA MATAJIRI DUNIANI 2018 Reviewed by By News Reporter on 3/08/2018 09:09:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.