Loading...
Katika dunia ya sasa kila mmoja anajitahidi kumiliki simu janja, lakini rais wa Urusi Vladimir Putin ameweka wazi kwamba yeye binafsi hatumii simu janja.
Rais Putin mwenye umri wa miaka 65 na anayeongoza taifa la watu milioni 144 aliyasema hayo Siberia siku alipokutana na wanasayansi na kushangaa kila mtu mfukoni mwake kulikuwa na simu janja (smartphone).
Alisema hana maslahi ya kujiunga na mitandao ya kijamii ya habari tofauti na mwenzake wa Marekani Donald Trump ambaye hutumia Twitter kama silaha yake binafsi ya kisiasa.
Rais Putin anaamini iwapo angekuwa anatumia simu janja (smartphone) basi simu hiyo ingeita kila mara. Pia, Rais Putin husoma dondoo za taaarifa rasmi tu kwenye mitandao ya kijamii ingawa yeye mwenyewe hajajiunga na mtandao wowote wa kijamii.
Mwaka jana alipokutana na watoto wa shule aliulizwa kama anatumia Instagram au mtandao wowote wa kijamii na alijibu kwamba binafsi hatumii na kwamba siku yake ya kazi ni ngumu na hukamilika mwishoni kabisa wa siku.
Siku za nyuma Putin aliwahi kusema kwamba Intaneti ni mradi maalum wa CIA.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za teknolojia punde zinapojiri.
RAIS WA URUSI NI KATI YA MARAIS WASIOTUMIA SMARTPHONE, JE NI KWANINI?
Reviewed by By News Reporter
on
3/08/2018 09:33:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: