Loading...
Serikali ya Japan imeamua kuwa roboti zitatumika kutoa huduma kwa asilimia 80 kwa wazee nchini humo mpaka kufikia mwaka 2020.
Gazeti moja nchini humo limechapisha habari ya kuwa kiwanda cha roboti nchini Japan kina mpango wa kuboresha roboti ili kurahisisha maisha ya wazee nchini humo kwa kutumia teknolojia.
Roboti hizo zitakuwa zikiwasaidia wazee kwa kuwatoa kwenye vitanda hadi kwenye viti vyao na vilevile kuwasaidia kwenye kuoga.
Dr Hirohisa Hirukawa, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Robot, Taasisi ya Taifa ya Sayansi ya Juu na Teknolojia amesema kuwa lengo lake kuu ni kurahisisha maisha ya wazee walio katika vituo tofauti na pia waliopo majumbani.
aliongezea kuwa ni asilimia nane pekee ya vituo vya kulelea wazee vinatumia roboti katika kutoa huduma zake.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za teknolojia punde zinapojiri.
ROBOTI KUTUMIKA KUHUDUMIA WAZEE NCHINI JAPAN
Reviewed by By News Reporter
on
3/08/2018 10:23:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: