Loading...

GUTERRES AZUNGUMZIA HAKI ZA WANAWAKE

Loading...
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia umuhimu wa haki sawa kwa wanawake ulimwenguni.

Gutteres katika kaudhimisha siku kuu ya wanawake duniani amesema kuwa kunyimwa kwa wanawake haki zao kunaathiri dunia nzima.

Amesisitiza kuwa jukumu la kutunza haki za wanawake ni kwa wanaume,vijana,wanawake na vilevile wasichana.

"Kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana ni  changamoto kubwa zaidi ya haki za binadamu duniani kote," alisema katibu mkuu.

Kulingana na Guterres, wanawake zaidi ya bilioni duniani kote hawana ulinzi wa kisheria dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia katika nchi zao.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.


GUTERRES AZUNGUMZIA HAKI ZA WANAWAKE GUTERRES AZUNGUMZIA HAKI ZA WANAWAKE Reviewed by By News Reporter on 3/09/2018 10:00:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.