Loading...

KOREA KASKAZINI NA MAREKANI KUFANYA MAZUNGUMZO NCHINI FINLAND

Loading...
Taarifa zilizotolewa na kituo cha habari cha Yonhap Korea Kusini zafahamisha kuwa  mazungumzo kati ya Marekani , Korea Kaskazi na Korea Kusini yanatarajiwa kufanyika  nchini Finland.

Kituo hicho cha habari cha serikali kimefahamisha kuwa Choe Kang Il mkurugenzi  msaidizi  amejielekeza  Jumapili nchini Finland akishirikiana  na wanadiplomasia wengine watatu kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Beijing.

Shirika hilo la habari la Yonhap limefahamisha kuwa Choe atashiriki katika  mazungumzo baina ya Korea Kaskazini, Korea Kusini na Marekani.

Kulingana na taarifa zilizotolewa  na vyanzo vya habari, ni kwamba  balozi wa zamani wa Marekani - Korea Kusini Kathleen Stephens, mwanadiplomasia wa zamani wa Korea Kaskazini na wasomi watashiriki katika mazungumzo hayo.
Na Catherine Kisese.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
KOREA KASKAZINI NA MAREKANI KUFANYA MAZUNGUMZO NCHINI FINLAND KOREA KASKAZINI NA MAREKANI KUFANYA MAZUNGUMZO NCHINI FINLAND Reviewed by By News Reporter on 3/20/2018 08:33:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.