Loading...

ZAIDI YA WAFUNGWA 700 WAACHIWA HURU KWA MSAMAHA WA RAIS - BURUNDI

Loading...
Takribani wafungwa mia saba arobaini,wengi wao walioshiriki maandamano ya kumpinga raisi Pierre Nkurunziza mnamo mwaka 2015 wameachiwa huru jana ijumaa nchini Burundi serikali imetangaza.

Wafungwa hao waliachiwa huru kutoka katika gereza kubwa zaidi la Mpimba jijini Bujumbura chini ya muongozo wa waziri wa sheria Aimee-Laurentine Kanyana, tukio lililoshuhudiwa na baadhi ya mabalozi wa mataifa ya magharibi.

Kuachiliwa kwao huru kunakuja baada ya msamaha wa raisi mwishoni mwa mwaka jana.

Wafungwa 450 kati ya 740 walishiriki katika harakati za uasi mwaka 2015 kumpinga raisi aliyeko madarakani alieleza waziri Kanyana.

Hata hivyo waziri wa sheria nchini Burundi Aimee-Laurentine Kanyana amewaonya wafungwa hao walioachiwa huru kutorejea kutenda makosa hayo kwani adhabu yake ni kifungo cha maisha.
Na Hamis Fakhi - Burundi.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
ZAIDI YA WAFUNGWA 700 WAACHIWA HURU KWA MSAMAHA WA RAIS - BURUNDI ZAIDI YA WAFUNGWA 700 WAACHIWA HURU KWA MSAMAHA WA RAIS - BURUNDI Reviewed by By News Reporter on 3/20/2018 08:52:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.