Loading...

KUNA SABABU NA KUSUDI KWA KILA HALI UNAYOPITIA KATIKA MAISHA - Na Siri ya Utajiri

Loading...
Kuna wakati tunapitia katika MATATIZO makubwa kiasi cha kuona kama dunia yote inakuelemea wewe tu. Wakati ambao unaona dalili za kufikia ndoto yako zinafifia, kila kitu unachokifanya unaona hakitoi matunda.

Watu wengi desturi yetu ni KULAUMU na KULALAMIKA kwa nini hali hii imetokea. Wengi wakati huu ndio ule muda ambao wanakata TAMAA na kupoteza MATUMAINI ya kufikia ndoto zako, wananza kuamini kuwa malengo yao hayawezekani tena.

Nataka nikueleze jambo moja ambalo litakusaidia utakapokutana na hali hii. Kuna SABABU na KUSUDI kwa kila hali inayotokea maishani mwako. Katika kipindi kigumu cha matatizo usipoteze matumaini na kulalamika. Kuna SOMO na jambo la muhimu kujifunza kutoka katika hali hiyo.

Matatizo ni sehemu ya kukujenga na kukufanya kuwa hodari japo yanaandamana na maumivu. Katika maumivu haya unatakiwa uwe pia na mtazamo wa kuangalia nini kusudi la kupita katika hali hiyo. Kuna kitu cha kujifunza katika kila changamoto.
Vicent Stephen

Tuma neno 'MAKALA' kwenda +255765112259 kupata makala za utajiri punde zinapojiri.
KUNA SABABU NA KUSUDI KWA KILA HALI UNAYOPITIA KATIKA MAISHA - Na Siri ya Utajiri KUNA SABABU NA KUSUDI KWA KILA HALI UNAYOPITIA KATIKA MAISHA - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 3/07/2018 01:59:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.