Loading...
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na ikulu ya rais mjini Bujumbura Jumapili, ni kwamba kura ya maoni kuhusu marekebesho ya katiba inatarajiwa kufanyika ifikapo Mei 17 mwaka 2018.
Tangazo kutoka ikulu limefahamisha kuwa vyama vya kisiasa, vyama vya ushirika na wanasiasa huru wanaojitegemea wanataraji kushiriki katika uchaguzi wanaombwa kujisajili kwa mamlaka husika kuanzia Machi 23 hadi Aprili 6 .
Burundi inajiandaa na uchuguzi mkuu wa mwaka 2020.
Katiba mpya inatarajiwa kuwa muhula wa rais kuongoza, muda wake utaongezwa kutoka miaka mitano na kuwa miaka 7.
Marekebesho hayo ya katiba tayari yanapingwa na upinzani kwa madai kuwa rais Nkurunziza atakuwa amepewa furs aya kuwa rais wa milele.
Na Hamis Shakhi - Burundi.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
KURA ZA MAONI KUHUSU MAREKEBISHO YA KATIBA BURUNDI KUFANYIKA MEI 17
Reviewed by By News Reporter
on
3/19/2018 06:30:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: