Loading...
Serikali ya Urusi imetangaza kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza, hali inayoendelea kuyumbisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi imesema wanadiplomasia hao wa Uingereza wana wiki moja kuondoka nchini humo.
Hatua hii ya Urusi imeonekana kama kulipiza kisasi baada ya Uingereza kuwafukuza wanadiplomsia wake 23 wiki hii.
Hii ilikuja baada ya uchunguzi kuonesha kuwa Moscow ilihusika katika jaribio la kumuua jasusi wake wa zamani Sergei Skripal na binti yake Yulia kwa kuwapa sumu hatari.
Pamoja na kuwafukuza wanadiplomasia hao, Urusi pia imefunga kituo cha kutoa mafunzo ya utamaduni wa Uingereza kufunga ubalozi wake mdogo mjini Saint Petersburg.
Urusi imeendelea kukanusha kuwa ndio iliyohusika na tukio la kumpa sumu, jasusi huyo wa zamani ambaye anaendelea kupata matibabu nchini Uingereza.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema, hatua ya Urusi haitabadilisha msimamo wa nchi yake kuwa, Moscow ndio iliyompa sumu jasusi huyo wa zamani wa Urusi na Uingereza.
Na Geofrey Okechi - Dar es salaam
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.

URUSI YALIPIZA KISASI KWA KUWAFUKUZA WANADIPLOMASIA 23 WA UINGEREZA
Reviewed by By News Reporter
on
3/19/2018 06:37:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: