Loading...

MAELFU WAANDAMANA KUDAI UDHIBITI WA SILAHA MAREKANI

Loading...
Katika ongezeko la kihistoria la uhamasishaji wa vijana kisiasa, maelfu ya vijana na wanaowaunga mkono wameandamana Marekani kote kudai udhibiti mkali wa silaha nchini humo, wakiapa kutumia nguvu ya kura kutimiza lengo.

Waliingia katika mitaa ya mji mkuu wa taifa hilo na miji mingine kama Boston, New York, Chicago, Houston, Minneapolis, Phoenix, Los Angeles na Oakland, California, katika idadi ambayo ilionekana wakati wa enzi za Vita vya Vietnam, na kuwazoa wanaharakati ambao kwa muda mrefu wamevunjwa moyo na mkwamo katika mjadala wa umiliki wa silaha na kuzijumuisha sauti nyingi mpya za vijana.

Walihamasishwa na viongozi wapya kabisaa: Wanafunzi manusura wa shambulio la shule mjini Parkland, Florida ambalo liligharimu maisha ya watu 17 Februari 4. "Ukisikiliza kwa karibu zaidi, unaweza kusikia watu walioko madarakani wakitetemeka," alisema manusura wa Parkland David Hogg mbele ya umati wa waandamanaji waliofurika mtaa wa Pennsylvania mita chache kutoka majengo ya bunge na karibu na ikulu ya White House.

"Tunalipeleka hili kwenye uchaguzi, kwa kila jimbo na kila mji. Tutahakikisha watu bora zaidi wanaingia na kugombea katika uchaguzi wetu, siyo kama wanasiasa lakini kama Wamarekani." Kwa sababu hii," alisema akinyoosha kidole nyuma yake kwa kuba la jengo la bunge, " hii haiwezi kukata shauri hilo."
Na Geofrey Okechi


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kimataifa punde zinapojiri.
MAELFU WAANDAMANA KUDAI UDHIBITI WA SILAHA MAREKANI MAELFU WAANDAMANA KUDAI UDHIBITI WA SILAHA MAREKANI Reviewed by By News Reporter on 3/25/2018 11:23:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.