Loading...

MAFANIKIO YAKO YA KESHO YANATEGEMEANA NA UNACHOKIFANYA LEO - Siri ya Utajiri

Loading...
Mafanikio yako ya KESHO yanategemeana na unachokifanya LEO, kwa lugha nyingine mafanikio ya kesho ni matunda ya matendo yako ya leo. Kwa hiyo ukitaka kuishi maisha yenye MAFANIKIO lazima LEO ufanye kitu ambacho baadaye kitakufanya uishi hayo mafanikio.

Kama kweli unamaanisha NIA yako ya kutaka MAFANIKIO basi ni vyema leo ufanye MAPITIO ya matendo yako ya SASA kuona kama yanaaksi hitaji lako la kuishi maisha ya mafanikio. Unachokifanya leo ndicho kinapaswa kuongea ili kubaini kama kesho utakuwa na mafanikio.

Ni kujidanganya sisi wenyewe pale tunapoishi kwa kutenda KINYUME na inavyopaswa huku tukiendelea kusubiri mafanikio. Katika yai la kuku kamwe huwezi kupata bata .UNACHOKIPANDA leo ndicho UTAKACHOVUNA.

Maisha yako ni ya muhimu sana kuyaacha yapite hivi hivi, hebu chukua muda kutathmini unachokifanya leo.

You Deserve The Best!
Vicent Stephen


Tuma neno 'SIRI YA UTAJIRI' kwenda +255765112259 kupata muendelezo wa makala punde zinapojiri.

MAFANIKIO YAKO YA KESHO YANATEGEMEANA NA UNACHOKIFANYA LEO - Siri ya Utajiri MAFANIKIO YAKO YA KESHO YANATEGEMEANA NA UNACHOKIFANYA LEO - Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 3/25/2018 01:56:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.