Loading...

MNYAMA MREFU ZAIDI AMEGUNDULIKA NCHINI SWEDEN

Loading...
Mnyama mrefu zaidi duniani amekutwa kuwa na sumu.

Watafiti nchini Sweden wamegundua kuwa mnyoo huyo mwenye urefu wa mita 55 ana sumu lakini sumu hiyo haina madhara yoyote  kwa binadamu.

Profesa wa chuo kikuu cha Uppsala nchini Sweden,Prof. Dr. Ulf Göransson wakati alipohojiwa na kituo che televisheni cha taifa amesema kuwa  utafiti kuhusiana na minyoo inayoishi katika hali ya baridi nchini humo umeoyesha kuwa minyoo hiyo ina sumu.

Kwa mujibu wa habari,inawezekaan siku za usoni minyoo hiyo ikatumika kutengeneza dawa.

Minyoo hiyo kwa lugha ya kirumi inaitwa "Lineus longissimus",na ina urefu wa mita 55-60.
Na Mohammed Makame.


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afya punde zinapojiri.
MNYAMA MREFU ZAIDI AMEGUNDULIKA NCHINI SWEDEN MNYAMA MREFU ZAIDI AMEGUNDULIKA NCHINI SWEDEN Reviewed by By News Reporter on 3/28/2018 08:58:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.