Loading...
Kata ya kwale, Mombasa nchini Kenya imekuwa kata ya kwanza nchini humo kufanikisha kukataza matumizi ya mirungi kama kilevi na biashara.
Uamuzi huo ulitangazwa siku ya Jumatano na Baraza la Kata hiyo baada ya wazazi na walezi kufikisha malalamiko kwamba namba kubwa ya vijana wao wanaaribika kutokana na matumizi ya mirungi.
Kwa kuongeza, baraza hilo la kata wamekuwa wakiona idadi kadhaa ya vijana ikikataliwa katika zoezi la usahili wa KDF (Jeshi la Ulinzi la Kenya) kutokana na meno ya vijana hao kuaribiwa na matumizi ya kilevi hicho.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) mirungi imeorodheshwa miongoni mwa dawa za kulevya zinazomfanya mtumiaji awe teja, ikiwa na maana ataendelea kuzitumia kila siku kiu kitapomshika.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
MOMBASA-KENYA: KATA YA KWALE YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIRUNGI
Reviewed by By News Reporter
on
3/08/2018 01:18:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: