Loading...

MTANDAO WA SNAPCHAT WALAZIMISHWA KUWAOMBA RADHI RIHANA NA CHRIS BROWN

Loading...
Mtandao wa Kijamii wa SnapChat umelazimika kuomba radhi kwa kusababisha kero baada ya kucheza tangazo linalokera likiuliza watumiaji wake kama wangepedelea "Kumpiga kofi Rihanna" au "Kumpiga ngumi Chris Brown".

Tangazo hilo, lilikuwa ni kumbukumbu ya kesi ya msanii Chris Brown mwaka 2009 alivyomshambulia mpenzi wake wa zamani kimwili, ambalo "lilihakikiwa na kupitishwa kimakosa".
Tangazo hilo linalokera liliondolewa mara baada ya kuonekana kuleta hisia mbaya katika mitandao ya kijamii.

Mwanaharakati wa Kimarekani, Brittany Packnett aliikosoa mtandao huo wa kijamii kwa kuruhusu tangazo hilo kuchezwa ambalo "Lilionyesha mwanga katika unyanyasaji wa kibinadamu"

Katika kauli ya Mashable, msemaji wa SnapChat alsema: "Tangazo lilikaguliwa na kupitishwa kimakosa, kutokana na kuvunja miongozo yetu ya matangazo. Tulilitoa tangazo hilo mapema mwisho wa juma lililopita, baada ya kugundua hilo. Tunaomba radhi wa kilichotokea."
Na Neema Joshua - Dar es salaam.

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MTANDAO WA SNAPCHAT WALAZIMISHWA KUWAOMBA RADHI RIHANA NA CHRIS BROWN MTANDAO WA SNAPCHAT WALAZIMISHWA KUWAOMBA RADHI RIHANA NA CHRIS BROWN Reviewed by By News Reporter on 3/16/2018 09:15:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.