Loading...

RATIBA YA AROBAINI YA MAREHEMU KINGUNGE NA MKEWE YATANGAZWA RASMI

Loading...
Kwa Niaba ya familia ya marehemu wazazi wetu Mr & Mrs. Kingunge Ngombale Mwiru naomba kuwasilisha kwenu ratiba ya arobaini ya wazee wetu wapendwa.

-Jumamosi tarehe 17/03/2018
(Kuanzia saa 11:00 jioni waombolezaji kufika nyumbani)
-Saa 1:00 jioni kuanza ibada mpaka tutakapohitimisha na baadae kupata chakula cha jioni pamoja.
-Baadae mkesha utaendelea usiku kucha hadi siku ya junapili saa 7:00 mchana kupata chakula cha pamoja na kuhitimisha rasmi msiba wa wazee wetu wapendwa.

Ukiwa ni ndugu, na rafiki wa karibu wa familia yetu uwepo wako kwenye shughuli hii utakua ni wa faraja mno kwetu sisi . 

ASANTENI sana kwa message zenu ambazo mmeendelea kutuma, na simu mlizoendelea kutupigia ni za faraja mno katika kipindi hiki kigumu sana. 

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.

Raha ya milele uwape Eh Bwana, Na Mwanga wa milele uwaangazie, wazazi wetu wapumzike kwa Amani!

Amen.
Na Geofrey Okechi - Dar es salaam


Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
RATIBA YA AROBAINI YA MAREHEMU KINGUNGE NA MKEWE YATANGAZWA RASMI RATIBA YA AROBAINI YA MAREHEMU KINGUNGE NA MKEWE YATANGAZWA RASMI Reviewed by By News Reporter on 3/16/2018 08:46:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.