Loading...

MKE WA DONALD TRUMP JR. ADAI TALAKA BAADA YA KUISHI KWA MIAKA 13

Loading...
Mke wa mtoto wa rais Trump ameamua kudai talaka mahakamani baada ya mwenendo wa maisha yake kubadilika kutokana shughuli za kisiasa zinazoendelea ndani ya familia yao.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti, Vanessa, mke wa mtoto mkubwa wa rais Trump mwisho wa siku ameamua kuomba talaka mahakamani baada ya mfarakano uliokuwa unaendelea chini chini kwa majuma kadhaa.

Chanzo karibu na mtandao wa TMZ umesimulia kwamba ugomvi wao ulianza chini ikidaiwa Vanessa alishachoshwa na matukio yanayoendelea katika familia hiyo yanayotokana na propaganda za kisiasa na sababu kubwa iliyomperekea kuchukua uamuzi huo ni pale alipotumiwa barua yenye unga wa poda wenye sumu. Pia mkwe huyo wa rais Trump kiujumla ameonyesha kutopendezewa na maswala ya siasa.

Wawili hao walioana mwaka 2005, wakibahatika kupata watoto watano Kai, Donald III, Spencer, Tristan na Chloe Trump. Lakini inaonekana tamati yao imefika.
Na Catherine Kisese - Dar es salaam

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
MKE WA DONALD TRUMP JR. ADAI TALAKA BAADA YA KUISHI KWA MIAKA 13 MKE WA DONALD TRUMP JR. ADAI TALAKA BAADA YA KUISHI KWA MIAKA 13 Reviewed by By News Reporter on 3/16/2018 08:31:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.