Loading...

WAPINZANI WAPINGA MABADILIKO YA KATIBA NCHINI BURUNDI

Loading...
Jukwaa la wapinzani waliopo ng'ambo ya Burundi 'CNARED' waliandaa mkutano kuanzia Machi 9 hadi 10 jijini Leuven, Ubeligiji, ili kuunda 'Jukwaa la Citoyen' ambalo litakusanya wanachama kutoka vyama pinzani, viongozi wa mashirika ya kijamii na waandishi wa habari waishio ng'ambo.

Malengo ya mkutano huo ni kuzungumzia namna ya kuzuia au kupinga kura za maoni ya katiba mpya iliyopangwa kufanyika Mei 2018, alisema Jean Minani mwenyekiti wa CNARED. "Kipindi hiki ni kibaya, na ni muda wa kufanya kazi kwa pamoja," aliwaambia washiriki katika mkutano.

Gabriel Rufyiri, mwenyekiti Shirika lisilo la kiserikali la OLUCOME linalopambana na rushwa ambaye alihudhuria katika mkutano huo alionyesha kujitoa katika 'Jukwaa la Citoyen' akilalamika kwamba kanuni za miko ya OLUCOME hazishabiriani na sera za 'Jukwaa la Citoyen'.

Alisema pia alihudhuria katika mkutano kwa sababu haungi mkono sera ya 'kiti wazi'. Rais Nkurunzinza ameonyesha kutaka kuendelea kubaki madarakani kwa kujaribu kubadili katiba ya nchi hiyo ili awe kiongozi wa maisha.
Na Hamis Shakhi, Gitega - Burundi

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za Afrika Mashariki punde zinapojiri.
WAPINZANI WAPINGA MABADILIKO YA KATIBA NCHINI BURUNDI WAPINZANI WAPINGA MABADILIKO YA KATIBA NCHINI BURUNDI Reviewed by By News Reporter on 3/16/2018 07:37:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.