Loading...

YANGA WAIBIPU SIMBA

Loading...
MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussein Niyika amesema endapo timu hiyo itaibuka na ushindi dhidi ya Township Rollers ya Bot­swana, basi Simba ijiandae ku­kumbana na kipigo kikali kwe­nye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Nyika alisema: "Tupo Botswana hivi sasa tukiendelea na mikakati yetu ya kuhakikisha tunawafunga Township Rollers lakini pia tunajiandaa na mechi yetu na Simba ambayo tutaku­tana nayo hivi karibuni.

"Hata hivyo, endapo tutashin­da mechi hiyo ya kesho basi Sim­ba wajiandae kwa kipigo kwani tutakuja kwa nguvu mpya katika mechi hiyo ya ligi kuu.

"Nasema hivyo kwa sababu vijana wetu wana ari lakini pia nguvu mpya ya kupambana to­fauti na awali."
Geofrey Okechi, Dar es salaam

Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za michezo punde zinapojiri.
YANGA WAIBIPU SIMBA YANGA WAIBIPU SIMBA Reviewed by By News Reporter on 3/16/2018 06:47:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.